24 Aprili 2015 - 07:49
 Marekani yakiri kuuwa mateka

Ikulu ya Marekani ya White House imekiri kwamba mateka kutoka Marekani na Italia wameuwawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani katika viwanja vya majengo yanayowahifadhi wapiganaji wa al-Qaeda nchini Pakistan mwezi Januari. Muda mfupi baada ya tangazo kutolewa

Ikulu  ya  Marekani  ya  White House imekiri kwamba  mateka kutoka  Marekani  na  Italia  wameuwawa  katika  shambulio  la ndege  isiyokuwa  na  rubani  katika   viwanja  vya  majengo yanayowahifadhi  wapiganaji  wa  al-Qaeda  nchini  Pakistan  mwezi Januari. Muda  mfupi baada  ya  tangazo  kutolewa, rais Barack Obama  alitumia  mkutano  na  waandishi  habari  katika  ikulu  ya Marekani  kuomba  radhi kwa  familia za  wahanga. Amesema anachukua  dhima  ya  operesheni  yote  ya  kupambana  na magaidi , ikiwa  ni  pamoja  na  hii, na  kwamba  ameamuru uchunguzi  kamili  wa  tukio  hilo. Wafanyakazi  hao  wawili  wa mashirika  ya  kutoa  misaada  waliouwawa  katika  mashambulizi hayo  ni Warren Weinstein , Mmarekani  ambaye alikamatwa  na  al-Qaeda  mwaka  2011, na  Mtaliani Giovani Lo Porto, ambaye alikamatwa  mwaka  mmoja  baadaye. Pia Mmarekani  mwanachama wa  kundi  la  al-Qaeda  aliuwawa  katika  shambulio  hilo.